Proverbs 24:30-34


30 aNilipita karibu na shamba la mvivu,
karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili,
31 bmiiba ilikuwa imeota kila mahali,
ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na
ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.
32Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona,
nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona:
33 cBado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:
34 dhivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi,
na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.
Copyright information for SwhNEN